Kanada kuanza kuuza bangi kwanzia Julai Mosi

Submitted on Thu, 06/01/2017 - 10:22

Chama tawala cha nchini Kanada, The Liberal Party of Canada leo kimepeleka musuada wa kuhalaisha bangi katika bunge la nchi hiyo ya Marekani ya magharibi.

Musuada huo  ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu sana tangu kampeni za uchaguzi mwaka 2015, ambapo Liberals waliaahidi wananchi kuwa, kama wananchi watawachagua kuongoza nchi, pale waiingiapo madarakani watahalalisha uuzaji, uvutaji na ulimaji wa bangi nchini Kanada.

Musuada huo utaruhusu yeyote yule mwenye umri wa miaka 18, na kuendelea kuwa na gramu 30 za bangi bila ya kuwa na hatia ya kupatikana na madawa ya kulevya.

Watumiaji na wavuta bangi pia wanaweza kuotesha miiche minee majumbani mwao kwa ajili ya matumizi yao ya binafsi. Na wale wanaotaka kununua wataweza kufanya hivyo kutoka dispensary maalum za bangi kote Kanada.